June 22, 2020


BAADA ya kikosi cha Simba kufika jijini Mbeya leo kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuvaana na Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itashuka Uwanja wa Sokoine, Juni 24 kumenyana na Mbeya City.

Mchezo huo utakuwa ni wa 31 kwa Simba sawa na Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Amri Said.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 75 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 18 na kibindoni ina pointi 30, zote zimecheza mechi 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic