June 24, 2020


JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa wana kazi ngumu kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambazo ni dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons ambazo ni dakika 180.
Leo Juni 24 itamenyana na Mbeya City kisha Juni 28 itakuwa na kazi ya kumenyana na Tanzania Prisons zote zitachezwa Uwanja wa Sokoine.
Bocco mwenye mabao matano kati ya 67 yaliyofungwa na Simba iliyocheza mechi 30 ndani ya Ligi ikiwa nafasi ya kwanza amesema kuwa watapambana.
“Tunatambua kuwa tutakuwa na mechi ngumu na zenye ushindani, hivyo tumekubaliana kufanya kazi kwa moyo mmoja kutafuta matokeo chanya kwani tunahitaji pointi tatu muhimu,” alisema Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic