MOHAMED Hussein, ‘Tshabalala’ ni mzawa ndani ya kikosi cha mabingwa ambaye amekuwa kwenye ubora wake kwa muda wa misimu mitano alipojiunga na Klabu ya Simba msimu wa 2014.
Tshabalala ni zao la Azam FC ambapo amedumu kuanzaia msimu wa 2014/15, 2015/16,2016/17,2017/18,2018/ 19 na sasa msimu wa 2019/20.
Simba ikiwa imefunga mabao 63 amehusika kwenye mabao manne licha ya kuwa ni beki akisema kuwa yote ni kutokana na kujituma kwa ajili ya kuona timu yake inapata matokeo.
Amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao ambapo mabao yake yote mawili amezifunga timu zenye majina ya Sugar.
Aliwatungua Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba bao lake la kwanza msimu huu kwa pasi ya Meddie Kagere na bao lake la pili aliwatungua Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri kwa pasi ya Jonas Mkude.
Tshabalala amesema kuwa sababu kubwa ya kuwa bora ni juhudi pamoja na kujituma bila kuchoka.
Yes, if you want to see the plains, you have got to climb the mountains
ReplyDeleteWafikishie Ujumbe Yanga
ReplyDeleteKwanini mpaka sasa hawajawaleta na kukamilisha idadi ya benchi lao la Ufundi? Safari za ndege zimefunguliwa siku nyingi Ulaya na sehemu nyingine lakini makocha wa Yanga bado hawajawasili hili ni doa...na wana siku 10 tu kabla ya kuanza kwa ligi daktari na Wachua misuli Kocha wa fitness na kocha mkuu wote wanatokea nje ya nchi lakini bado hawajaripoti kambini...wakati Azam Kocha wao wamemfanyia njia ya haraka na sasa amewasili na anaendelea na program....Yanga yale madudu na virusi vinavyorudisha nyuma maendeleo bado vipo? Tafadhali sana hili lirekebishwe!