June 28, 2020



TUNAONA mambo mengi kwenye mpira wetu kwa sasa mambo ambayo yanaendelea uwanjani sio sawa kuona yakiendelea kila siku kwenye soka letu.
Burudani ya soka ilikuwa imekosekana kwa muda mrefu hivyo mashabiki na wadau walikosa kwa muda uhondo, kurejea kwakwe wamepokea kwa shangwe ila ghafla mambo yanaonekana kuwa tofauti.
Kila timu imeweka mipango yake ya kufikia kwenye mechi ambazo wanacheza lakini hayawezi kuendelea kwenda sawa ikiwa hakutakuwa na usawa na maamuzi makini.
Ukitazama kwa sasa mechi ambazo zimebaki kwa timu nyingi ni kuanzia saba hivyo hesabu zikigoma kwenye mechi moja tayari zinatibua ratiba nzima.
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuona kwamba haki inatendeka na kila timu inashinda kwa haki bila malalamiko yoyote hiyo ndio zawadi kwa mashabiki pamoja na viongozi wa timu.
Matokeo yanayoumiza ni yale ambayo timu haikustahili kuyapata na ikapata hii ni mbaya kwani jambo ambalo linatakiwa kufuatwa kwa sasa ni sheria 17 kwenye maamuzi.
Iwapo maamuzi hayatakuwa mazuri basi itakuwa ngumu kumpata mshindi halali na ubaya ni kwamba iwapo maamuzi yakishapita ndani ya dakika tisini hayabadiliki milele licha ya adhabu kutolewa.
Tunaomba mamlaka husika zinazosimamia masuala ya michezo kwa sasa kuongeza umakini mkubwa kwenye mechi za ligi zote ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Ligi Daraja la Kwanza.
Kwenye Ligi Kuu Bara balaa kubwa ambalo linapasua kichwa ni kwa timu kushuka daraja na kuona namna gani wanaweza kubaki kwa msimu ujao.
Timu 10 hazina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao hapo  unapata picha namna gani ushindani ulivyo na namna ambavyo ukitibua hesabu ya mtu mmoja tu anapotea jumla.
Dakika 90 zimeshikilia ushindi na ukubwa wa pointi tatu ambazo zitaweza kumfanya mshindi abaki ndani ya ligi ama aporomoke kwenye ligi.
Kinachotakiwa ni kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa umakini bila kujali ni mazingira gani anapitia katika kazi yake hiyo muda huo.
Jambo pekee ambalo litatoa picha ya matokeo mazuri ni maandalizi bora kwa kufuata kanuni za mpira huku wachezaji wao wakiwa tayari kwa ajili ya kupambana ndani ya uwanja.
Kundi kubwa ambalo linahaha kutafuta nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao linapambana kuona namna gani wanaweza kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.
Hakuna ambaye anaweza kutabiri kwa sasa nani anaweza kushuka daraja kwa kuwa kila timu inauhakika wa kubaki kwenye ligi kutokana na uwezo wa wachezaji wao.
Kikubwa kilichopo ni umakini katika kila jambo ambalo linafanyika kwa sasa kwani kushuka daraja ni jambo baya ambalo hakuna anayependa kuliona.
Licha ya kwamba ni jambo baya na hakuna anayependa kuona likitokea ni lazima iwe hivyo kwani ndio maisha ya soka yalivyo na kikubwa ni kuzingatia kanuni katika kila jambo.
Nina amini kuwa mambo yanafanyika hivyo ili kila timu ikiwa inacheza ikubumke kuleta ushindani wa kweli na kuacha kufanya utani kwenye kazi ambayo wanaifanya hivyo kikombe cha kushuka hakiepukiki.
Ikiwa mamlaka husika ambazo zinasimamia michezo kwa sasa namaanisha Shirikisho la Soka nchini,(TFF) itaongeza umakini katika kila hatua nina amini timu zitashuka kiuhalali na zile ambazo zitapanda pia zitapitia njia halali.
Kwa timu ambazo zimekuwa zikiingia na matokeo uwanjani nadhani zimevuna kile ambacho zimekipanda hasa wanapokuja kushtuka kwamba ushindi waliotarajia unakwenda kwa mpinzani wake.
Muhimu kila timu ikatambua kwamba mshindi ni yule anayepatikana ndani ya uwanja. Dakika tisini huwa haziongopi lakini lazima kanuni na utaratibu ufuatwe.
Kwa zile timu ambazo zinafikiria kubaki ndani ya ligi ni lazima zipambane kweli ili kushinda mechi zilizobaki ili kujiepusha na kikombe cha kushuka daraja.
Pia ni muhimu TFF wakaongeza waangalizi maalumu kwenye mechi zilizobaki kwa sasa kuanzia ligi kuu pamoja na Ligi Daraja la Kwanza kwani kuna hali ya hatari inakuja hapo baadaye iwapo hakutakuwa na uangalizi maalumu.
Zile ambazo zinaona zinakaribia kushuka huwa zinapoteza matumaini ya kucheza kwa ushindai jambo ambalo linaua ule ubora wa ligi.
Ndani ya Ligi Daraja la Kwanza kwa zile timu ambazo zina nafasi ya kupanda daraja huwa zinaamua kutumia mbinu ambazo sio nzuri hasa kwenye mechi za nyumbani kwa kutoa vitisho kwa wapinzani.
Hii ni mbaya ikiwa itatokea na tunaweza kupoteza sasa ladha ambayo ilikuwa ipo wakati ule kabla ya janga la Corona na kuanza kushughulikia masuala mengine ninapenda kuziomba timu zote zitulie ili hali isifikie huko.
Ulimwengu wa soka unapenda kuona amani na utulivu vinaendelea ndani ya uwanja na kila mshindi anashinda kwa uhalali na sio ujanjaujanaja ama kutumia fursa ya kuwa mwenyeji kumuumiza mgeni.
Ninaamini kwamba kila timu itatumia vema mechi ambazo zimebaki kwa sasa kusaka ushindi huku wale ambao wanajipanga kupanda ligi wakipambana kupata ushindi katika kutafuta matokeo ndani ya uwanja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic