JOHN Bocco,
nahodha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba ameweka rekodi ya dakika
180 kwenye mechi mbili ambazo wamecheza hivi karibuni kwenye viwanja viwili
tofauti.
Juni 17, Bocco
mwenye mabao saba kibindoni alianza kuweka rekodi ya kwanza Uwanja wa Taifa
ambapo alihusika kwenye mabao mawili wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya
Mwadui FC , alifunga bao moja na kutoa pasi moja kwa Hassan Dilunga.
Mchezo wa
pili ilikuwa ni Juni 24, Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo Bocco alihusika kwenye
kufunga mabao yote mawili wakati Simba ikishinda mabao 2-0.
Ndani ya
dakika 180, Bocco amefunga mabao matatu viwanja viwili tofauti na kuhusika
jumla kwenye pointi sita ilizotwaa Simba, ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 78
na imetupia mabao 69.
Hii ni baada ya masuala ya michezo kuruhusiwa kuendelea kwani hakukuwa na masuala ya michezo tangu Machi 17.
Sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona ambalo linaivuruga dunia ila kwa Tanzania, Serikali iliridhia masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa masuala ya michezo yanaweza kuendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment