June 4, 2020


KLABU ya Chelsea imepanga kuwapelekea chakula wachezaji wake ndani ya gari baada ya mazoezi ili kujenga miili yao kutokana na sheria ya kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima kuendelea.

Sheria hiyo ina lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vilisababisha kusimamishwa kwa shughuli nyingi duniani ikiwa ni pamoja na michezo.

Kwa sasa matumizi ya kanteen kwa wachezaji pamoja na wafanyakazi yamekatazwa jambo ambalo limewafanya viongozi kufikiria mbinu mbadala ya kuwapa chakula wachezaji wao wanaojiandaa na kurejea kwa Ligi Kuu England Juni 17.

Imeripotiwa kuwa wakati Kocha Mkuu, Frank Lampard akiwa anakinoa kikosi chake wapishi watakuwa jikoni wakipika na kuweka msosi ndani ya gari la kila mchezaji ambao ataufinya na mwingine kwenda nao nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic