KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas amesema kuwa kuna uwezekano wa Simba na Yanga zikakutana kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho iwapo kila mmoja atashinda mechi zake.
Simba na Yanga zimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Azam FC, ratiba inaonyesha Juni 27/28 Simba itacheza na Azam FC ikiwa itashinda itakutana na mshindi wa mchezo kati Yanga itakayocheza na Kagera Sugar.
Abbas alisema kuwa kutokana na ushindani uliopo kwenye Kombe la Shirikisho inawezekana Simba na Yanga zikakutana hivyo ni lazima utaratibu wa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ukazingatiwa kwa mashabiki kuingia nusu.
“Inawezekana, Simba na Yanga zikakutana kwani kuna mashindano ya Kombe la Shirikisho,Serikali imeruhusu mashabiki kuingia uwanjani kwa kuzingatia muongozo ambao umetolewa, kwa mechi ambazo zitakutanisha mashabiki wengi kama Simba na Yanga hapa ni lazima mashabiki waingie nusu.
“Lengo letu ni kuona kwamba tunaendelea kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona kwani licha ya kwamba tumejiridhisha maambukizi yamepungua bado Corona ipo na tahadhari ni lazima ichukuliwe,” alisema Abbas.
Chanzo:Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment