June 8, 2020



DK.Rashid Seif Mfaume, mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, jana aliongoza jopo la wataalamu kuweza kutembelea makao makuu ya Azam FC kutazama miundombinu kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea kuendelea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ilisimamishwa Tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.



Dk.Mfaume aliambatana na Ofisa Afya Manispaa ya Temeke, Rehema Sadick, Ofisa Afya Manispaa ya Ilala, Reginald Mlay, pamoja na uongozi wa juu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA), ikiwa ni Katibu Mkuu wake Msanifu Kondo na Mkurugenzi wa Mashindano Daudi Kanuti.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Dk. Mfaume, ameelezea kuridhishwa na namna Azam FC ilivyojipanga.:-"Nimeridhishwa sana na uwekezaji mlioufanya katika upande wa tahadhari dhidi ya Virusi hatari vya Corona.

"Huu mtambo mlioufunga hapa ni wa aina yake, kwa kweli mnastahili kuwa mfano kwa viwanja vingine kama Taifa na Uhuru.

"Jambo tunalopenda kusisitiza tu kuwa makini katika kuwakumbusha mashabiki wanaokuja hapa kuzingatia kuweka umbali (social distancing) baina yao."


Meneja wa Uwanja huo, Sikitu Kilakala, amesema klabu imekuwa ikifanya kila kitu kwa miongozo ya Serikali kupitia Wizara ya Afya, na iko tayari kuendelea kupokea maelekezo ili kuhakikisha watu wote wanaofika uwanjani wanakuwa salama na kurudi majumbani kwao salama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic