June 7, 2020


PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa watapambana mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa inahitaji ushindi ili kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael inatarajia kukutana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali utakaopigwa kati ya Juni 27/28 Uwanja wa Taifa.

Tshishimbi amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa mchezo wa kwanza waliokutana nao kwenye ligi walifungwa jambo litakalowafanya waongeze umakini.

“Kagera Sugar ni timu nzuri ilitupa changamoto tulipokutana nao kwenye mchezo wa ligi, kwa kuwa haya ni mashindano mengine tutapambana ili kupata ushindi ukizingatia kwamba tutakuwa tumecheza mechi nyingi baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza.

“Malengo makubwa ya wachezaji na timu kiujumla ni kubeba kombe la Shirikisho hivyo njia pekee ya kulipata ni kushinda mchezo wetu kisha mengine yatafuata baadaye,” amesema Tshishimbi.

Yanga ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuanza kuinyoosha mabao 4-0 Iringa United, Uwanja wa Uhuru, Desemba 21 mzunguko wa 62, ilishinda 2-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, mzunguko wa 32, Januari 26 na ilishinda mbele ya Gwambina kwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru hatua ya 16 bora Februari 26 iwapo itapenya kiunzi cha robo fainali itakutana na mshindi kati ya Simba ama Azam FC hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic