ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa atapambana na Mbao FC iliyopamba moto ndani ya Ligi Kuu Bara kwa tahadhari ili kupata ushindi.
Mtibwa Sugar imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Alliance FC kwenye mchezo wao uliopita na leo inakutana na Mbao FC ambayo imetoka kushinda mabao 2-0 mbele ya Lipuli FC.
Katwila amesema kuwa hajapata muda wa kuwatazama wapinzani wake ila anaamini ni timu imara ndio maana imepata ushindi kwenye mechi zake zilizopita ila hilo halimpi hofu.
"Tunamchezo dhidi ya Mbao FC ambao wapo vizuri kwani timu ikitoka kushinda ina maana kwamba ina uwezo mkubwa lakini jambo moja ambalo nasi tunalihitaji ni pointi tatu muhimu.
"Wachezaji wapo tayari kwani matokeo ambayo tumeyapata nyuma hayakuwa mazuri lakini ndio masuala ya mpira dakika tisini zinaamua mambo yaweje," amesema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imekusanya pointi 38 huku Mbao FC ikiwa nafasi ya 19 na pointi zake 32.
0 COMMENTS:
Post a Comment