July 17, 2020


TIMU ya Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba imecheza jumla ya mechi 17 ugenini ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20.

 Kwenye mechi hizo, Azam FC imeshinda mechi 7 ambazo ni dakika 630 na imekusanya sare nne huku ikiambulia kichapo mechi sita.

Mchezo wake uliopita ugenini ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila na kuifanya ikusanye jumla ya pointi 25 ugenini.

Ina kibarua cha kumenyana na Lipuli Julai 19 Uwanja wa Samora kwenye mchezo wa ligi.

Ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65 inakutana na Lipuli iliyo nafasi ya 16 na pointi 40 zote zimecheza mechi 35.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Azam FC inapambania nafasi ya pili ndani ya ligi huku Lipuli ikipambana kupata nafasi ya kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic