UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kiungo wao Mghana, Bernard Morrison asitegemee wao kutangaza kuvunja mkataba wake huku wakisisitiza kuwa mchezaji huyo bado ni mali yao mwenye mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kukipiga Jangwani.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Mghana huyo kuondoka uwanjani wakati timu hiyo ikiendelea na mchezo wake wa Nusu Fainali ya Kombe la FA walipocheza na Simba na kulala kwa mabao 4-1, baada ya kutolewe katika dakika ya 64.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela,amesema kuwa kiungo huyo bado ni mali yao hadi Julai 15, 2022, baada ya kuongeza mkataba wake wa miaka miwili.
Mwakalebela alisema kuwa kiungo huyo kama anafanya matukio ya kiutovu wa nidhamu kwa makusudi akitegemea uongozi utasitisha mkataba wake na kuondoka kama mchezaji huru, basi imekula kwake.
Aliongeza kuwa kiungo huyo ataondoka kwenye timu hiyo mara baada ya mkataba wake kumalizika huku ukimtaka kutumia njia nzuri na sahihi ya kutaka kuondoka kwenye timu na siyo kufanya vituko.
“Sisi Yanga wala hatuna shida na Morrison, kikubwa kama anataka kuondoka ni vema akatumia njia zilizokuwa sahihi na siyo kufanya vituko akiamini sisi tutatangaza kuachana naye.
“Hivyo basi anatakiwa kufahamu kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili.
“Hatutakuwa tayari kuachana naye hadi pale timu itakayomhitaji kutufuata kukaa meza moja kufikia makubaliano mazuri ya kuuvunja mkataba wake wa miaka miwili,” alisema Mwakalebela.
Chanzo: Championi
Duh!gongo wazi poleni
ReplyDeleteHao ndio GONGOWAZI wanahangaika sana na huyo mchezaji wao inaonekana ndio tegemeo lao kubwa sana
ReplyDeleteOnja joto la jiwe
ReplyDeleteAmezowea kuchezea timu kwa mkataba wa mara moja na si kuurejea (renew the contract) tena. Aliopewa unaisha mwisho wa msimu huu kwa hiyo kwake Morrison ndiyo mwisho pia wa kuichezea Yanga. Tatizo Yanga hawakumjua hivyo licha ya kumsajii akiwa kama mchezaji huru. Hawakujiuliza mchezaji bora vile aliwezaje kukaa bia timu ya kuchezea?
ReplyDeleteyani hizi timu mbovu kweli maana wanafanya mambo yasiyofaa kabisa bora kuzifuta na kutoshiriki ligi yetu wanatutia aibu sana halafu ni timu kubwa kama yanga
ReplyDeleteViongozi wapo sahihi atafanya mazoez tu miaka2
ReplyDeleteBwana mke akikukataa hata pindi ikiwa unampenda kupindukia kiasi na umemtolea mahari ya mamilioni na ikiwa mwenye heshima yako basi umwache na akikwambia hautaki nawe mwambie Nami sikutaki Mara kumi na umpe talaka kabla ya kukufanyia mchafu mbele yako akueke pabaya au pia kukudhuru na hiyo ndio sifa ya muungwana kama ni muungwana kweli. Yeye atakuwa amekaa tu lakini si lazima madhali ni mchezaji wenu mumpe mishahara na matumizi ya Nyumba, sasa nani atayehssurika?
ReplyDeleteMtapata shida wenyewe kwa sababu kodi ya nyumba mnaendelea kumlipia, mshahara mnaendelea kumlipa lakini hachezi. Maana yake anawazibia nafasi ya idadi ya wachezaji wa kigeni. Hivi hamkujiuliza mchezaji wa kiwango cha Morrison akose timu hadi mumsajili akiwa huru?
ReplyDeleteKwani ni mara ngapi wachezaji wanasajiliwa wakiwa huru? Hao mliowachukua kutoka azam akina boko,nyoni nk au alivoondoka okwi nao si walitoka wakiwa huru ina maana nao walikua ovyooo
ReplyDelete