July 2, 2020


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama akaamkia kulia kisha Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck akampanga atokee upande wa kushoto hapo utajua uzuri na ubaya wa Simba.

Chama amesema kuwa upande ambao anapenda kucheza upande wa kushoto kwa kuwa ni sehemu ambayo anapenda kucheza muda wote.

Akiwa ndani ya uwanja akipoa kwa dakika mbili, Simba inapoa kwa muda wa dakika tano na akibanwa kabisa basi hapo kuna yale makali ya Simba hayataonekana.

Bado ana kazi kubwa ya kuthibitisha ubora wake kwenye dabi dhidi ya Yanga kwani mbele ya Azam FC huwa anachezea mpira namna anavyotaka na kuifanya timu icheze mpira wa pasi nyingi.

Clatous Chama ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa ni namba moja kwenye kutengeneza mipira ya mwisho ambapo ametengeneza pasi nane.

Simba ikiwa imefunga mabao 69 yeye ana mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara na bao lake jingine alifunga jana Julai Mosi mbele ya Azam FC, Uwanja wa Taifa.

Simba inakwenda kukutana na Yanga kwenye hatua ya nusu fainali ikiwa utakuwa ni mchezo wa wazi tutashuhudia ufundi mwingi licha ya kwamba dabi ya Yanga na Simba huwa haitazami nani ana kikosi bora bali dakika 90 hushikilia matokeo ya mchezo mzima.

11 COMMENTS:

  1. Huyo Chama anashindwaga kucheza mechi ya Yanga akikutana na Tshishimbi na Fei Toto. Jana nimeangalia gemu yao na Azam, Simba hawana uwezo wa kuifunga Yanga kwa sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We ndimu kweli yani kushinda hiko kimechi kimoja ndo unaleta kibnuri umefungwa miaka mitano mfululizo ushindi wako ulikuwa droo leo mnajiona mna uwezo wa kuifunga Simba kila mara mtajuta safari na ninavyowajua nyinyi kuna mgogoro mkubwa tunaenda kuutenegeneza hiyo tarehe kumi na mbili uchawi haunaga muda mrefu.

      Delete
  2. Na walioangalia gemu ya yanga na kagera watasemaje hamna timu zaidi ya kubebwa na refa

    ReplyDelete
  3. Yanga Hana timu ya kuifunga Simba,

    ReplyDelete
  4. Simba haiwezi kuifunga Yanga kwa sasa. Simba walikuwa wanashinda kwa sababu ya wale mamluki waliotoka Simba na kusajiliwa Yanga. Yanga haina mamluki tena. Mziki mtauona.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msije mkapigana tu manake ndo staili zenu sasa hivi mpira uwanjani dakika tisini hatutaki mpigane nyie kwa nyie.

      Delete
  5. Gemu hii wanaanza wote Banka, Tshishimbi, Fei Toto na Haruna wale viungo wenu watapigana siku hiyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na Makame Bui kama holding midfielder.

      Delete
    2. Huyo haruna alikuwepo Yanga ilipofungwa 5-0 na simba, Tshishimbi toka aje Yanga ana ushindi mmoja tu dhidi ya simba hao wengine sisemi tarehe 12 hicho kidomo chenu mtakifunga na migogoro mtaianza

      Delete
  6. Yanga inaelekea inaandaa timu ya kujilinda dhidi ya simba tar 12. Lakini bila nguvu ya ziada yanga lazima afungwe. Na siku houp refa alete zake aone. Labda ile timu yao ya kamati ya ufundi toka gamboshi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic