CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana hiyana iwapo atahitajika kukipiga ndani ya Yanga kwani kazi ya mchezaji ni kucheza mpira.
Chama amekuwa kwenye ubora wake msimu huu wa 2019/20 kwa upande wa kutengeneza pasi za mwisho ambapo anazo jumla 11 na amefunga mabao sita.
Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa Yanga inahitaji kupata saini ya nyota huyo ikiwa na lengo la kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao.
Chama amesema:" Kwa mchezaji kazi yake ni kucheza bila kujali yupo wapi ila kikubwa ni utaratibu kufuatwa kwani kwa sasa nipo ndani ya Simba.
"Bado nina mkataba na Simba kwa timu ambayo itakuwa inahitaji saini yangu ni lazima iwasiliane na uongozi wa Simba," amesema.
Ukenda huko kwa jinsi hali ilivo, tegemea kuzomewa wakati wowote kama yanavowakuta Molinga na Morrison na hapo majuto mjukuu
ReplyDeleteStory zenu za Morison zimebuma mnaanza kutunga uzushi mwingine
ReplyDeleteHuu ni UZUSHI wa 4G. Hii interview ya lini?Ujinga wa kujaribu kuleta uzushi ili kubalance watu wasahau 4G.
ReplyDeleteMwandishi huna jipya. Mchezaji mzuri na mwenye akili hawezi kutoka simba kwenda yanga kwa sasa. Labda aende nje ya nchi hii. Yanga wajipange kwanza waache kuendesha timu kwa style ya kuwazuga mashabiki wao
ReplyDeleteKwanza hii stori ilishaandikwa humu wakati ule makamu mwenyekiti wa yanga alipodai kuwa wameshamalizana na Chama kuhusu kujiunga nao
DeleteHana Jipya huyu mwandishi, na 4G,inakuuma kwelikweli
DeleteNdugu zangu, Chama si mageni hapa hali iliyopo. huko kwengine Anaaijuwa vizuri na akili zake tamamu. Yeye hapo ni kuwainjoy na waanze kuuota. na hakuna jengine. Wasimchezee myama, atawaliza tena
ReplyDeleteChampioni kateni rufaa na Utopolo wenu.4G ndio habari ya mujini. Hata mkijaribu kubadili reli haitasaidia. Nice try though.Wamerudishiwa salaam loud and clear katika masafa ya 4G.
ReplyDeletehawaoni hata aibu wao habari zao kusomwa ni kuleta uzushi au habari mbaya kwa Simba wakati ule ilikuwa muuaji wa simba kila ukifungua page mbona hamjaandika muuaji wa yanga vyura nyie
ReplyDeleteUchungu wa utopolo kufungwa na Simba hata kuweka update imekuwa ngumu
ReplyDeleteStori zenu za morison zimeisha sasa mmeanza za chama kweli akili mmeshikiwa kandambili aka vyura aka GONGOWAZI
ReplyDelete