JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ametumia dakika 450 kukiongoza kikosi chake kwenye mechi za Ligi Kuu Bara bila kuambulia pointi tatu huku akifungwa mabao saba na kufunga mabao matatu jambo lililomsikitisha kocha huyo.
Tangu Machi 17 hakukuwa na mechi za ushindani kutokana na janga la Corona, mchezo wake wa mwisho kabla ya masuala ya michezo kusimamishwa ilikuwa ni Machi 10 ambapo aliinyoosha Lipuli FC mabao 2-0, Uwanja wa Mkwakwani.
Tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea na kwa sasa ikiwa imecheza jumla ya mechi tano ambazo ni dakika 450 ilikuwa ikisaka pointi 15 imeambulia pointi mbili baada ya kulazimisha sare mbili huku ikipoteza pointi 13 jumlajumla.
Ilianza Juni 13, kulazimishana sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Mkwakwani. Juni 20,ikatoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar,Uwanja wa Mkwakwani.
Juni 23,ikaifuata Mbao FC ikapigwa bao 1-0.
Juni 27,ikakutana na Alliance FC ikanyooshwa bao 1-0 zote ilikuwa Uwanja wa Kirumba, Mwanza.
Juni 27,ikakutana na Alliance FC ikanyooshwa bao 1-0 zote ilikuwa Uwanja wa Kirumba, Mwanza.
Juzi,Julai 6, ilikubali kichapo cha cha mabao 3-1 mbele ya Mbeya City 3-1 Uwanja wa Sokoine.
Coastal Union ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 33 kesho ina kazi ya kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine. Haina presha ya kushuka daraja lakini ikipoteza mechi zake zilizobaki hatakuwa ndani ya tano bora kwa kuwa timu nyingine zina uwezo wa kufikia pointi zake 48.
0 COMMENTS:
Post a Comment