July 18, 2020

DODOMA Jiji leo wameibuka Mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Julai 18.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Anuary Jabir dakika ya 52 kwa guu la kulia ndani ya 18 na kumshinda mlinda mlango wa Gwambina FC.

Gwambina imetinga hatua ya fainali baada ya kukata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 kutoka kundi B.

Dodoma FC ilikuwa kundi A ambao nao tayari wameshakata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Bao la Jabir linakuwa la 11 ndani ya Ligi Daraja la Kwanza akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi hiyo.

Mbwana Makatta, Kocha Mkuu wa Dodoma FC amesema kuwa wapinzani wake Gwambina walikuwa imara katika kumiliki mpira ila wameshindwa kumaliza nafasi ambazo wamezitengeneza.

Fulgence Novatus, Kocha Mkuu wa Gwambina amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa na kila mmoja akipambana kupata matokeo licha ya makosa madogo kutoka kwa waamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic