July 6, 2020


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha jana, Julai 5 wakati wakikubali kugawana pointi moja na Biashara United.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Shecky Mganzija amesema kuwa Niyonzima hakuumia sana hivyo leo anaweza kuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzanke.

Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Julai 8.

"Niyonzima hajaumia sana hata leo anaweza kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar," amesema.

Niyonzima amefunga jumla ya mabao mawili ndani ya Yanga ambapo amefunga bao moja kwenye ligi na bao moja kwenye Kombe la Shirikisho.

1 COMMENTS:

  1. Bodi ya Ligi inatumika kisiasa na inaihujumu Yanga kwanini mabadiliko ya ratiba ya mechi dhidi ya Kagera kuchezwa saa 9 mchana....hapa unajiuliza kwanini ili lifanyike kwa haraka haraka kiasi hicho? Tunaelewa mikakati ya kisayansi ya kuidhoofisha Yanga. Amani itatoweka na wahusika watafikishwa kwa Mheshimiwa Raisi ambaye anasimamia maslahi ya wanyonge na haki na usawa kwa wote....tunawajua wenye nia ovu na mikakati ya chuki kwa Yanga!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic