July 6, 2020


USHINDI wa bao 1-0 walioupata Namungo mbele ya JKT Tanzania ambao waliitungua Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroeck, Februari 7 bao 1-0 imewapa hali ya kujiamini kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya mabingwa hao utakaopigwa Julai 8, Uwanja wa Majaliwa.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Abeid Athuman dakika ya 34 na kuwafanya Namungo inayonolewa na Hitimana Thiery kusepa na pointi tatu jumla.Itakutana na Simba kwenye mchezo wao wa pili ambapo baada ya mchezo huo kutakuwa na sherehe za Simba kukabidhiwa kombe lao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wanatambua mchezo wao unaofuata dhidi ya Simba, Julai 8 utakuwa mgumu kwa kuwa wanacheza na mabingwa ila wachezaji wake wamepata hali ya kujiamini.
“Unapozungumzia kucheza na bingwa sio kitu chepesi, tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa wana kikosi kizuri na wachezaji makini lakini inapofika kwenye suala la pointi tatu nasi tunazihitaji pia hivyo sherehe yao itakuwa na upinzani mkubwa tunajipanga kuona namna gani tutapata ushindi mapema,” amesema.
Kwenye mchezo wa kwanza waliokutana Uwanja wa Taifa, Namungo iliyeyusha pointi tatu kwa kufungwa mabao 3-2 na Simba hivyo itaingia uwanjani ikiwa na roho ya kisasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic