LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anafanya maombi ili kiungo wake Haruna Niyonzima awe fiti Julai 12 Kwenye mechi dhidi ya Simba, Uwanja wa Taifa.
Yanga itamenyana na Simba, Jumapili hii Kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya mchezo dhidi ya Sahare All Stars na Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Eymael amesema kuwa amelazimika kufanya hivyo kutokana na hali ya kiungo huyo kutoeleweka mpaka sasa baada ya kupata jeraha la goti kwenye mechi dhidi ya Biashara United iliyopigwa Uwanja wa Karume.
Aliukosa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison dakika ya 79 kwa pasi ya David Molinga .
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa kikubwa anachokifanya ni maombi ili mchezaji wake awe fiti Julai 12.
"Niyonzima uwepo wake Kwenye mechi yetu dhidi ya Simba ninachokifanya kwa sasa ni maombi tu ili awepo kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba kwani hali yake haieleweki,"
0 COMMENTS:
Post a Comment