July 8, 2020


WAZIR Junior, mshambuliaji namba moja ndani ya Mbao FC leo amefunga bao pekee la ushindi kwa timu yake mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Kirumba ambapo Mtibwa Sugar imekubali kufungwa bao 1-0 dakika ya 63 na kuyeyusha pointi tatu jumla.

Bao hilo leo ni la 11 kwa nyota huyo ambaye amekuwa kwenye ubora wake akiwa amefunga mechi yake ya pili mfululizo ambapo alitoka kuipa ushindi timu yake kwenye mechi dhidi ya Lipuli FC kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Jr amesema kuwa kikubwa kinachowabeba kwa sasa ni juhudi na kujituma ili kuweza kulinda nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

Mbao ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 34 imebakiwa na mechi 4 kukamilisha mzunguko wa pili. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic