July 11, 2020


 KUELEKEA dabi ya Jumapili, itakayopigwa Uwanja wa Taifa, kati ya Simba na Yanga mabosi wa Simba wameweka ahadi  ya Sh Mil 400 kwa wachezaji wake huku Yanga wakiweka mezani sh Mil 200.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Championi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji pamoja na viongozi wake wameweka ahadi ya Sh Mil 400 kwa wachezaji wake kama watafanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga.

Hivyo katika mgawo huo kila mchezaji atayecheza ataondoka na sh Mil 20,watakaotokea benchi sh Mil 10 watakaokaa benchi bila kucheza sh Mil 7,huku wale ambao hawatacheza wataambulia sh Mil 5.

Kwa upande wa Yanga kampuni ya GSM wameweka ahadi kama ile ya kwanza ya Sh Mil 200 huku kukiwa na nyongeza ya ahadi kama watafanikiwa kuifunga Simba.

Hivyo kama Yanga watafanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo kila mchezaji atayeanza atafanikiwa kuvuna Sh Mil 10,wachezaji wa akiba watapata Sh Mil 5 na wale watakaokaa jukwaani watapata Sh Mil 2.

3 COMMENTS:

  1. Hizi timu zina majina makubwa lkn viongozi uozo mtupu,ahadi za nini na mnawalipa mishahara?halafu mkichelewa kuwapa mishahara wanagoma kucheza,siku msipo waahidi watacheza chini ya kiwango..acheni ujinga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic