July 28, 2020


INAELEZWA kuwa kocha wa zamani wa Yanga Hans Pluijm anakuja kubeba mikoba ya Mbelgiji Luc Eymael ndani ya Yanga.

Eymael amefukuzwa kazi ndani ya Yanga kutokana na vitendo vyake vya kibaguzi jambo ambalo limepelekea uongozi wa Yanga kuamua kuachana naye.

Julai 26 baada ya kumaliza ligi kwa kuishusha Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Samora kwa ushindi wa bao 1-0 ilisambaa sauti yake akisema kuwa hafurahishwi na mambo yanayofanyika ndani ya Tanzania pamoja na mashabiki kutokujua masuala ya soka.

Habari zinaeleza kuwa tayari Yanga wamefanya mawasiliano na Pluijm ili kurejea tena ndani ya Bongo kukinoa kikosi hicho.

"Tayari kwa sasa uongozi umeanza kufanya mawasiliano na Hans, mambo yakiwa sawa anaweza kutua ndani ya Bongo kukinoa kikosi cha Yanga," ilieleza taarifa hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga,Simon Patrick amesema kuwa masuala ya benchi la ufundi yanashughulikiwa kwani ni mapema kwa sasa shughuli ya kwanza ni kuondoka kwa Eymael.  

6 COMMENTS:

  1. Wameshamlipa pesa anazowadai pia wana uwezo wa kumwekea dst na wifi na kumpa gari ya kutembelea

    ReplyDelete
  2. Yakale Ni dhahabu! utopolo wanahaha na kukurupuka now! now!

    ReplyDelete
  3. Zahera ndie anaewafaa yanga kutokana na hali yao.jamaa kawasidia yanga kwenye ziki walipopata nafuu yanga wakamfukuza zahera. Puljim ni chaguo la mkwasa. Ndie aliemfanyia figisu zahera..Yanga majungu matupu hawawezi kupiga hatua wasipobadilika.Yanga hawana vyanzo vya uhakika vya kuendeshea timu na hata hicho kidogo kinachopatikana kuna wezi wanaiba pale na ndio maana wakamfukuza zahera kwa sababu alitaka kujua kila kinachopatikana na matumizi yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic