July 28, 2020

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema kuwa yupo tayari kuwajibishwa na uongozi wa klabu hiyo kufuatia mwenendo mbaya katika ligi kuu msimu huu.

Katwila amesema anastahili hata kujiuzulu au kufutwa kazi kama viongozi watafikia uamuzi huo, ingawa mara zote dhamira yake ilikuwa ni kuiongoza Mtibwa Sugar katika kuyafikia malengo ya kufanya vizuri katika kila msimu.

2019/20 ulikuwa msimu mbaya zaidi kwa Mtibwa Sugar kuwahi kutokea tangu timu hiyo ilipopanda kucheza ligi kuu kwa kuwa ilikuwa miongoni mwa timu ambazo hazikuwa na uhakika wa kusalia katika ligi mpaka iliposhinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shoting, Uwanja wa Gairo.

 Katwila amesema: “Nipo tayari ‘ku-resign’ (kujiuzulu) kwa sababu ya matokeo mabaya, kama kocha ninatakiwa kuiongoza timu kushinda. Malengo yangu na ya kocha yeyote kwenye timu ni kuhakikisha anaipa mafanikio timu katika kila msimu, lakini mambo yamekuwa tofauti kwangu kwa msimu huu, kwa hiyo nipo tayari kufutwa kazi kama viongozi wataamua hivyo.” 

Chanzo: Championi

1 COMMENTS:

  1. HUYU COACH NI MZALENDO NA MSEMA KWELI , NASI TUNAMWAMBIA KUFANYA KOSA SI KOSA BALI KURUDIA KOSA NDIO KOSA . HIVYO VIONGOZI WA MTIBWA SUGAR MFIKIRIE SUALA HILI PALE MTAKAPOTOA UAMUZI .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic