KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison, leo maamuzi yake yanatarajiwa kutolewa na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kuhusu suala la mkataba wake ndani ya Yanga.
Jana, Julai Mosi, Morrison aliitwa TFF kuhojiwa ambapo habari zinaeleza kuwa ni kutokana na ishu ya mkataba wake ndani ya Klabu ya Yanga.
Mvutano mkubwa wa Yanga na Morrison ni ishu ya mkataba wake ambapo Morrison anasema kuwa dili lake alisaini la miezi sita na Yanga wanasema kuwa amesaini kwa muda wa miaka miwili.
Pia nyota huyo alisema kuwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara akiwa hajapewa mkataba ndani ya Yanga.
Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa kiungo huyo amethibitisha kuwa alicheza mechi mbili bila kuwa na mkataba.







Saleh ushabiki wa simba unakuponza hadi kutoka nje ya weredi wako,inawezekanaje kucheza bila leseni ya TFF ambayo hutolewa baada ya kupitia mikataba yote>?
ReplyDeleteApo safi sana lazima ukweli ujulikane maana hii imekuwa movie ya kihindi so leo tuone nani mkweli kati ya yanga vs morisoni, morisoni kaamuwa kuwa panda yanga badala ya kupanda juu ya mpira 😂😂😂
ReplyDeleteMuda wa Morrison kucheza mpira Tanzania unaonesha umefikia kikomo.
ReplyDeleteMorrison analitukana soka la Tanzania kama si dharau.
sio Morrison anayetukana soka la Tanzania!Ni Yanga ndiyo inatukana wachezaji wake na tayari Moringa alikuwa ameanza kutukanwa isingekuwa mechi za hivi karibuni amekuwa akiiokoa Yanga ikitokea nyuma kusawazisha naye hali yake ilikuwa mbaya
ReplyDeleteHizo mechi mbili alizocheza bila mkataba yanga wanyang'anywe pointi Morison anafumua uozo wa TFF
ReplyDeleteWw mpira huujui wala sheria za kawaida za mpira huzijui...mchezaji kabla hajaingia uwanjani kuna kuwa na ukaguzi wa leseni ya kufanya kazi...kamisaa wa mchezo husika lazima apitie...sasa angewezaje kucheza bila leseni acha ushabiki...kama unazitaka hizo point zichukue ww ukatumie nyumbani kwako.....
DeleteTff ndo huwa wanatoa leseni hizo...je!tff walimpa leseni mchezaji ambae hana mkataba?
DeleteWangeyamalizana kimyakimya na inaonesha ni kweli aliecheza hiyo miezi miwili Bila ya mkataba na Yanga haijakanusha kwa hilo hivo wamejipeleka kitanzini wenyewe
ReplyDeleteMsisimame kishabiki akuna mtu anae weza fanyakazi bila poshoo.na Morison asingewezacheza bila mkataba yanga nidhahir kabisa na kama hana mkataba na yanga ane mwambia avaee jezi yayanga nani wakati yupo huru same time mjifikilie .....Morison anafanya ujinga na soyanga ... Punguzeni kuwa namawazo finyu
ReplyDeleteNamna Yanga imekuwa ikicheza na kufanikiwa katika hizi mechi chache zilizopita ni dhambi..Azam alinyimwa magoli na penalt na sasa angekuwa nafasi ya pili.Namungo amefungwa goli la pili ambalo ni clear offside ya wazi..Cha kushangaza katika mechi ya Kagere Mwamzi alikuwa karibu na akina Kaseke faulo ilifanyika nje mchezaji wa Yanga kaangukia nje..Dhuruma na ujanja ujanja hautaifikisha Yanga mbali..Ni mabingwa wa historia lakini wanafika wapi ikifika michuano ya kimataifa?Na ndiyo timu pekee Tanzania ilishawahi fungiwa sababu ya rushwa ya kununua marefaree..Tunatumaini waamuzi watabadilika kuelekea mwisho wa ligi na mechi za FA zilizobakia
ReplyDeletewatu wanajifanya wanasahau kuhusu historia ya yanga na rushwa au sijui ni vitoto vya juzijuzi labda tuwakumbushe viongozi wa yanga walifungiwa CAF kwa kutaka kumhonga refa
DeleteDuh umenikumbusha hiyo ilikuwa mwishoni miaka ya 1980 Mzee Issa Makongoro na wenzake wawili walishikwa red handed na briefcase yao pale hoteli ikiitwa Embassy hotel.Wakapigwa ban ya 5 yrs au maisha wasishughulike na soka.Ilikuwa aibu kubwa.Sishangai kusikia Morisson alicheza mechi mbili bila ya mkataba na hapa msala unawaangukia TFF wanaotoa leseni
Deletekinachoendelea Yanga saa hii ni upangaji wa matokeo kuelekea ukingoni mwa ligi.Ingekuwa vizuri Takukuru wakachukua hatua
ReplyDeleteIssa Makongoro akiwa katibu mkuu wa Yanga alifungiwa maisha kwa kuhonga marefa kutoka Ethiopia.Yanga ndio ina historia ya kuhonga marefa kwa hukumu hiyo.
ReplyDeletehistioria hujirudia !Inawezekana kweli kasaini miezi sita wao wanafoji eti ni miaka miwili.Imekuwa kawaida dhuruma kwa makocha na wachezaji! Pondamali anadai haki yake ya miaka miaka mingi.Lwandamila... Zahera.,Dante katumia miezi mingi kudai mil 40, Beno Kakolanya...Hassan Kessy kudai haki...wakamfurushia virago dakika chache kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.Yondani ndiye anawajulia...Sasa Morrison atatembea juu ya vichwa vyao.
ReplyDeleteTFF please tendeni haki kwa wachezaji please ni aibu kubwa jamani huyu mchezaji ni mmoja tu kajitokeza wapo wengine
ReplyDelete