UONGOZI wa Simba umesema kuwa shukran kubwa za kutwaa ubingwa wanazirejesha kwa Mungu pamoja na mashabiki wa Klabu hiyo kwa kuipa sapoti mwanzo mwisho.
Leo Simba imekamilisha safari ya kukabidhiwa ubingwa wao Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majliwa.
Mchezo huo umekamilika kwa sare ya bila kufungana na kuwafanya Simba wasepe na pointi mbili nyanda za juu Kusini baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya bila kufungana na Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anaamini ni mpango wa Mungu kutwaa ubingwa pamoja na sapoti kubwa ya mashabiki.
"Wamekuwa nasi bega kwa bega mashabiki kwenye kazi kubwa ambayo wachezaji walikuwa wakifanya kwa namna yoyote ile wanahitaji pongezi na wanastahili haya tunayoyapata kwa sasa," amesema.
Huu ni ubingwa wa 21 kwa Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck, na Kocha Msaidizi Seleman Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment