MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wametua Dar wakitokea Lindi ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.
Kwenye mchezo huo uliochezwa jana, Julai 8 Simba ilitoshana nguvu na Namungo kwa kumaliza dakika 90 bila kufungana bao na baada ya mchezo huo wachezaji walikabidhiwa medali pamoja na kupewa kombe lao rasmi.
Kombe hilo linakuwa la kwao jumla kwa sasa kwa kuwa wametwaa mara tatu mfululizo hivyo kwa mujibu wa kanuni linakuwa mali yao.
Ilianza kutwaa msimu wa 2017/18, 2018/19 na msimu huu wa 2019/20.
Hili linakuwa ni taji lao la 21 la ligi kutwaa na leo wameanza msafara kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuelekea makao makuu ya Simba, Msimbazi wakilionyesha kombe kwa mashabiki ambao wamejitokeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment