KOCHA Mkuu
wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa ni tatizo kubwa kwake kuwakosa nyota wake
watatu ambao ni chaguo lake la kwanza.
Yanga
itamenyana na Simba, Julai 12 Uwanja wa Taifa huku kukiwa na hatihati ya kukosa
huduma za nyota wake hao watatu ambao ni Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu, Papy Tshishimbi anahitaji kufanyiwa upasuaji
wa goti na Mapinduzi Balama alivunjika mfupa mdogo kwenye mazoezi wakati Yanga ilipokuwa inajiaandaa kuvaana na Ndanda FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa bado hajajua
atafanya nini kwa sasa kutokana na wachezaji wake hao kutokuwa kwenye ubora.
“Ni tatizo kubwa kwa sasa kutokuwa na Tshishimbi, Niyonzima
na Balama, kwangu mimi nina amini ni wachezaji muhimu ila sina chaguo la
kufanya.
“Ninachokifanya ni kuendelea kuwatazama wachezaji ambao nipo
nao pia usiku ninafikiria kujua hali zao itakuaje, ila ninadhani kwa Niyonzima
inawezekana akaanza kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba itategemea hali yake
itakuaje,” amesema Eymael.
Kwenye mchezo wa jana wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Eymael alicheza bila ya wachezaji hao na alishinda bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison.
Si kasema atamuombe Mungu apone
ReplyDeletemwandishi acha kaz ni julai 8 au 12?
ReplyDelete