LEO kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho, Julai 8 dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo Yanga imemshusha kiungo wake, Mohamed Issa,'Mo Banka' ambaye alikuwa nje ya timu kwa muda mrefu.
Sababu kubwa ilikuwa inaelezwa kuwa Banka hakupewa stahiki zake ila kwa sasa wamemalizana na mabosi wake.
Pia sababu nyingine ya kiungo huyo kuwahishwa ni kukosekana kwa kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu hivyo kuna hatihati ya kukosa mchezo mwingine wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba Julai 12.
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa itakuwa ni ngumu Kwake kucheza bila ya Niyonzima ila wachezaji wake watapambana kupata matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment