July 7, 2020

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kumenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa.

Simba itashuka uwanjani kesho Julai 8, ikiwa imetumia dakika 180 kucheza bila kushinda zaidi ya kulazimisha sare ya bila kufungana.

Alianza Mbeya, Uwanja wa Sokoine,  Juni 28 kwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons kisha Julai 5 ikamalizana na Ndanda dakika 90 bila kufungana na kuambulia pointi mbili kati ya sita.

Sven amesema:" Kila kitu kipo sawa na wachezaji wana morali kubwa ya kupambana nina amini utakuwa mchezo mzuri na wa ushindani. 

"Wapinzani wetu wapo vizuri tunawaheshimu ila nasi pia tunahitaji kupata matokeo mazuri ni muhimu pia kwetu."

Hitimana Thiery Kocha Mkuu wa Namungo amesema wapo tayari kupata matokeo Kwenye mchezo huo wa kesho.

"Tupo tayari kuona namna gani tunaweza kupata matokeo, kila kitu kipo sawa kwa kuwa wachezaji wapo tayari, " amesema .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic