July 16, 2020


SIMBA leo imebanwa mbavu mbele ya Klabu ya Mbao FC kwa kukubali kichapo cha mabao 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, leo Julai 16.

Mbao ilianza kuibuka kwenye lango la Simba dakika ya 5 baada ya kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim kutema mpira uliokutana na guu la Rajab Rashid dakika ya 5.

Iliwabidi Simba wasubiri mpaka dakika ya 35 ambapo waliandika bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao namba moja Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti.

Bao hilo halikudumu kwani Mbao iliongeza msumari wa pili dakika ya 45+2 kupitia kwa Wazir Jr na kuwafanya Simba waende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1 huku Mbao ndio wakiwa wataalamu wa mchezo.

Kipindi cha pili kiungo mshambuliaji wa Simba Miraji Athuman aliweka usawa dakika ya 52 ila bao hilo lilidumu dakika saba wakatunguliwa Simba bao jingine tena dakika ya 59.

Jordan John dk 59 alìwanyanyua mashabiki wa Mbao FC na kuwafanya wasepe na pointi tatu mbele ya Simba wakiwatungua mabao mengi kwa msimu huu ambayo ni matatu.


Licha ya ushindi huo Mbao FC wanabaki nafasi yao waliyokuwa kabla ya kucheza na Simba ya 19 wakiwa wamecheza mechi 35 kibindoni wana pointi 38 wanapambana kujinasua na hatari ya kushuka daraja.

Simba pia wanaongeza idadi ya michezo ya kufungwa na kufikia minne kwa sasa wakiwa pia wamecheza mechi 35 na pointi zao 81 wakiwa tayari ni mabingwa.

3 COMMENTS:

  1. Kikosi kipana cha Simba kimeonyesha ubora wake leo #Haji Mnara

    ReplyDelete
  2. roho inakuuma chukua kamba jinyonge chuura fc 4g inawahusu

    ReplyDelete
  3. Sal kufungwa kwa Simba hakubadili lolote. Wanacheza kukamilisha ratiba. Lakini kipigo cha 4G kimewakosesha uwakilishi.Lazima roho ikuume.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic