July 12, 2020





Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amefunguka kuwa, anaamini ataifunga tena Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwa kuwa wanataka kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Simba na Yanga zinatarajia kupambana leo Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi atatinga fainali kuwania taji hilo ambalo lina tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Eymael amefichua kuwa malengo yao ni kuona wanapata ushindi katika mchezo huo licha ya kuamini wapinzani wao watakuja kwa lengo la kutaka kulipa kisasi kufuatia kuwafunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Machi 8, mwaka huu.

“Kitu kikubwa tunachokiangalia ni kwamba tunaweza kuibuka na ushindi katika mchezo wetu dhidi ya Simba, najua utakuwa mchezo mgumu kwa sababu wao watakuja kwa lengo la kutaka kulipiza kisasi, lakini kwa upande wetu tutakuwa tunahitaji ushindi.

“Sisi tunaangalia zaidi nafasi ya kwenda kushiriki michuano ya kimataifa na ndiyo maana hatuoni sababu za kupoteza mchezo huu kwani kwetu una umuhimu mkubwa, uzuri tunaenda kucheza na timu ambayo tunaijua vizuri ingawa michezo ya dabi huwa ina ugumu wake ingawa kitu cha msingi kwetu tunachotegemea ni ushindi tu,” alisema Eymael.


Kabla ya leo timu hizo kukutana, zimeshakutana kwenye Ligi Kuu Bara mara mbili msimu huu. Matokeo ya mechi hizo ni; Simba 2-2 Yanga na Yanga 1-0 Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic