HARUNA Niyonzima kiungo wa Yanga amesema kuwa ameomba acheze angalau kwa dakika 45 kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa Uwanja wa Taifa.
Niyonzima hakucheza mechi iliyopita ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 baada ya kuumia goti kwenye mchezo wa ligi mbele ya Biashara United.
Mtu wa karibu wa Niyonzima amesema kuwa kiungo huyo ameomba apewe dakika 45 ili afanye makeke yake ndani ya Uwanja licha ya kuwa ni majeruhi.
"Niyonzima ameomba dakika 45 ili azitumie kwenye mchezo dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa, sababu kubwa ya kuomba kufanya hivyo ni mapenzi na timu yake ya Yanga na anahitaji kutimiza majukumu yake kwa kuipeleka timu fainali ya Kombe la Shirikisho, " alisema mtu huyo.
Niyonzima amesema kuwa:"Bado ninaumwa ila nipo tayari kuipambania timu yangu kwa namna yoyote,".
Mshindi wa mchezo wa leo fainali atakutana na Namungo FC ambayo ilishinda jana, Julai 11 mbele ya Sahare All Stars Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Hizo ni mbwembwe tuu, atakuwa anatafita kick
ReplyDeleteKipindi cha mavuno hiki. Mdhamini anamwaga mzigo. Hakuna mchezaji ataekubali kuwa mgonjwa asilimia 100.
Delete