July 2, 2020


BERNARD Morrison leo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa wa chuo cha Sheria, Dar es Salaam. 

Morrison alikuwa kwenye mvutano na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake jambo ambalo lilipelekea awe nje kwa muda.

Yeye alikuwa anasema kuwa ana mkataba wa miezi sita huku Yanga ikieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

 Suala hilo lilitinga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo alihojiwa jana na kutoa maelekezo yake.

Ameingia Kwenye rekodi za wageni waliofunga Kwenye dabi kwani aliwatungua bao 1-0 Simba walipokutana Uwanja wa Taifa, wanatarajiwa kumenyana Julai 12. 

12 COMMENTS:

  1. Muuaji? ina maana hiyo simba imekufa? We mwandishi vipi siyo wote wanaofuatilia hii blog magonyolo

    ReplyDelete
  2. Mmmh Inaonekana mpaka leo Kuna mashabiki hawahui Lugha za kimichezo,

    ReplyDelete
  3. Huyo kanza kushabikia mpira ukubwani na inawezekana ndio mwaka wake wa kwanza ndio maana hajui maana ya muuwaji angekuwa anajua asingesema hivyo

    ReplyDelete
  4. Huyu si muuwaji wa Simba Bali ni muuwaji wa Yanga. Simba huyo sio mchezaji wake na wala Hakuna Alaaka na sio waliomleta wala waliomtolea gharama

    ReplyDelete
  5. Simba acheni woga. Mkisikia mnacheza na Yanga moyo unawaenda mbio. Ubingwa wenu wa magumashi. Mnapigwa tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Matokeo ya Yanga ndiyo yamekuwa ya magumashi...Mechi Yanga dhidi ya AZAM tunajua nani alibebwa. Yanga na Namungo tunajua nani alipewa goli la wazi la kuotea. Yanga na Kagera ile penalti kaangalie mechi haikuwa penalti haikuwa halali. Jana Man City kuifunga Liverpool haimaanishi Man City ni bora ya Liverpool. Kama Yanga ni bora basi itarudi na pointi sita toka kanda ya ziwa

      Delete
  6. Na kutokana na woga wake ndio wakachukuwa ubingwa Mara tatu mfululizo na itaendelea kwa miaka ijayo

    ReplyDelete
  7. Pengo la zaidi ya point 20 mtu bado anasema ubingwa wa magumashi, punguza kujifariji, huna timu ya kupambana na simba

    ReplyDelete
  8. Uwe unaenda uwanja au vibanda umiza uangalie mechi za simba na zile za yanga utapata majibu ni timu ipi insstahili ubingwa, sio kusubiri akina nugaz wakudanganye, wao wanalipwa kwa kueneza uongo ili mtulie

    ReplyDelete
  9. huwa inatokea klabu bora kufungwa..Simba ilipomfunga yanga 6 msimu huo Yanga ilikuwa bora zaidi. Na pia hata pale Yanga ilipocharazwa 5-0 bado wao ndiyo ilikuwa bora kisoka zaidi. Jana uingerezwa mabingwa Liverpool wametandikwa 4-0..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic