July 14, 2020

UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa una kazi kubwa ya kupambana na Simba kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela. 

Namungo FC ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars uliochezwa Julai 11, Uwanja wa Mkwakwani.

Itamenyana na Simba anbao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Bara waliopenya hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga.

Kocha Mkuu wa Namungo FC,  Hitimana Thiery amesema kuwa anatambua kuwa kuna kazi kubwa kupambana na mabingwa kwenye mchezo wao wa fainali. 

"Sio kazi nyepesi kushinda mbele ya mabingwa ambao wapo vizuri na tunawaheshimu kwa kuwa tunawatambua vizuri wapinzani wetu na wanajua kile wanachokifanya. 

" Nilikuwepo uwanjani kuona namna ambavyo walikuwa wakipambana ndani ya uwanja, ila hilo halinipi presha nitakiandaa kikosi kipate ushindi, " amesema.

3 COMMENTS:

  1. Hata siku moja huwezi kuisoma simba . mtabadilishiwa viungo wachezeshaji wakawepo shibobu , kichuya , miraji na kanda . Hapo usomaji bado upo?

    ReplyDelete
  2. Mmeanza kuwaaminisha Namungo ili nao waweze kusambaratishwa tena.

    ReplyDelete
  3. Ajitahidi maana wenzake wamenyolewa tiari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic