MTUPIAJI namba moja ndani ya Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Felix Minziro, Wazir Jr amesema kuwa kikubwa kinachombeba ni kufuata maelekezo ya mwalimu pamoja na ushirikiano wa wachezaji.
Mbele ya Mtibwa Sugar alifunga bao pekee la ushindi lililowapa pointi tatu muhimu Mbao mchezo uliochezwa Uwanja wa Kirumba.
Jr amesema kuwa amekuwa kwenye ubora kutokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji pamoja na kujituma.
"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila mmoja anatoa ushirikiano kwangu pamoja na wachezaji wenzangu nami pia ninafurahi ninapoona timu inapata matokeo," amesema.
Wazir Jr amefunga jumla ya mabao 11 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa na pasi tatu za mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment