July 6, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa  kiungo wake Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, atakosa mechi mbili muhimu kutokana na kuwa na majeraha ya goti.

Niyonzima ambaye amekuwa kwenye ubora wake tangu ajiunge na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Rwanda alipata jeraha hilo jana kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Karume ulikamilika kwa sare ya bila kufungana huku Niyonzima akitoka na kumpisha Abdulaziz Makame.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa Niyonzima atakosa mchezo dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Julai 8, Uwanja wa Kaitaba.

"Niyonzima hatakuwa kwenye kikosi kitakachocheza na Kagera Sugar kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha.

"Kwenye mchezo wetu muhimu dhidi ya Simba, Julai 12,inategemea itakuwaje hali yake."

Yanga ipo nafasi tatu ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 33 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nane ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 33.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic