MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo, Simba wameanza maandalizi ya kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Julai 8 dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.
Simba jana, Julai 5 ilimalizana na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Nagwanda Sijaona.
Kwenye mchezo huo timu zote zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
Inakutana na Namungo FC ambayo imetoka kuinyoosha bao 1-0 JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 3-2 hivyo Namungo ina kazi ya kulipa kisasi kwenye mchezo huo.
Namungo haina cha kupoteza kwani ina uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao baada ya kujiwekea kibindoni pointi 59 baada ya kucheza mechi 33.
Ikiwa nafasi ya 4 inakutana na Simba yenye pointi 80 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 33.
Ni Simba ndio haina cha kupoteza kwasababu ni tayari bingwa ama Namungo wanataka nafasi ya vipi unasema hawana Hawana cha kupoteza
ReplyDelete