July 17, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kichapo walichopokea cha mabao 3-2 kutoka kwa Mbao FC kimetokana na wachezaji wake kuwafunga watani zao wa jadi Yanga.

Julai 12, Uwanja wa Taifa Simba ilishinda mabao 4-1 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali. Ushindi huo umeipa nafasi Simba kutinga hatua ya fainali inayotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Sumbawanga.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Mbao wanastahili pongezi kwa kile walichokifanya na kupata ushindi mbele yao jana, Julai 16.

"Mbao wanastahili pongezi kwa kuwa wamefanya kazi kubwa ila kwetu sisi naamini mchezo wetu uliopita baada ya kushinda umekuwa ni mwendelezo kwetu kushindwa kufurukuta kwenye mechi zinazofuata.

"Lakini licha ya kupoteza bado sisi ni mabingwa na tumetwaa ubingwa huo tukiwa na mechi mkononi hivyo tunastahili heshima pia," amesema.

Mbao FC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi 35 huku Simba ikiwa kileleni na pointi 81.

1 COMMENTS:

  1. Kikosi B ndio kilicho cheza tunasubiri tarehe 2 tuchukuwe kombe letu FA tumalize kazi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic