July 28, 2020

RASMI sasa Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam umebadilishwa jina na utaitwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Leo, Julai 28,2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema hayo wakati akitoa hutoba kwenye maombolezo ya kumuaga Benjamini William Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu aliyetangulia mbele za haki.


Magufuli amesema :"Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo, kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, na kwakuwa nimepata meseji nyingi nimekubali na natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic