July 28, 2020


MANCHESTER United inatajwa kuendelea kumpigia hesabu nahodha wa Klabu ya Aston Villa, Jack Grealish kwenye dirisha la usajili msimu huu.

Mmiliki mwenza wa Aston Villa, Nassef Sawiris inaripotiwa kuwa ametaja dau la nyota huyo kuwa ni pauni milioni 80 ikiwa wanahitaji saini yake.

Mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England, mbele ya West Ham, Julai 26 kwenye sare ya kufungana bao 1-1, staa huyo anayemuongoza Mtanzania, Mbwana Samatta alifunga bao kwa Villa liliwaongezea nguvu ya kubaki ndani ya ligi hiyo pendwa.

Villa wanahitaji kiwango cha mchezaji huyo kuwa sawa na nyota wa kikosi cha United Harry Maguire ambaye naye alisajiliwa kwa dau la pauni milioni 80 akitokea Leicester City.

Dean Smith, Kocha Mkuu wa Villa amesema kuwa mtazamo wa Grealish unamtegemea yeye mwenyewe kile atakachosema anahitaji.

Mbali na United ambao wanahitaji saini yake pia Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola nayo inatajwa pia kuiwinda saini ya nyota huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic