REAL Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane imeshinda taji la La Liga la 34 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Villareal uliochezwa Uwanja wa Alfredo do Stefano.
Karim Benzema alitupia mabao mawili dakika ya 29 na la ushindi dakika ya 77 kwa mkwaju wa penalti huku lile la Villarreal likipachikwa na Vicente Iborra dakika ya 83.
Madrid imetwaa taji hilo ikiwa imeshinda jumla ya mechi 10 mfululizo jambo linalowafurahisha mashabiki pamoja na benchi la ufundi la Real Madrid.
Zidane amesema kuwa ilikuwa ni ngumu kufikia mafanikio jambo ambalo linampa furaha pamoja na wachezaji wake.
"Ligi ina jumla ya mechi 38 na ni ngumu kwangu kushinda ila kwa haya yaliyotokea ni ushindi mkubwa kwetu," amesema.
Real Madrid imetwaa ubingwa ikiwa imebakiza mechi moja mkononi na ina pointi 86 ambazo hazitafikiwa na mpinzani wake Barcelona mwenye pointi 79 wote wakiwa wamecheza mechi 37.
0 COMMENTS:
Post a Comment