ASTON Villa inayoshiriki Ligi Kuu England ambapo nyota Mtanzania, Mbwana Samatta anakipiga imepoteza matumaini ya kubaki ndani ya Ligi hiyo baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na Everton.
Mchezo huo ulikuwa na maana kubwa kwa Villa endapo wangeshinda na kusepa na pointi tatu wangejiongezea nafasi ya kubaki ndani ya ligi.
Wachezaji na benchi la ufundi baada ya mchezo hawakuwa na furaha kwa kuwa waliyeyusha matumaini ya kubaki msimu ujao wa 2020/21 ikiwa ni pamoja na kipa Pepe Reina.
Sare hiyo inaifanya Villa ibaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31 huku Everton ikiwa nafasi ya 11 na pointi 46 zote zimecheza mechi 36.
Villa walianza kupachika bao dakika ya 72 kupitia kwa Ezri Konsa likasawazishwa dakika ya 87 na Theo Walcott.
0 COMMENTS:
Post a Comment