July 15, 2020


SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeweka wazi mapato ya mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA kati ya Simba na Yanga, ambao umeingiza jumla ya Sh milioni 269 kwa tiketi ambazo ziliuzwa.

Katika mchezo huo ambao ulipangwa kuingiza mashabiki 30,000 ikiwa ni nusu ya mashabiki 60,000, walitakiwa kuingia kutokana na kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na virusi vya Corona.

Mauzo ya tiketi za mchezo huo yalisimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni baada ya kumalizika kwa mkataba wa kampuni ya Selcom ambayo ilikuwa kihusika na kuuza tiketi za mechi ambazo zinachezwa kwenye uwanja huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF katika mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, ambapo jumla ya mashabiki 22,990 waliokata tiketi waliingia.

Katika jukwaa la VIP A ziliuzwa tiketi 93 sawa Sh milioni 2,790,000, wakati VIP B zilizouzwa zikiwa ni 1,520 sawa Sh milioni 38,000,000 na VIP C, zilizouzwa tiketi 1,454 sawa Sh milioni 29,080,000 huku mzunguko zilizokuwa zimeuzwa zikiwa ni tiketi 19,923 sawa Sh milioni 199,230,000 iliyopelekea kuwa jumla ya Sh milioni 267,100,000 ambazo zimepatikana kwenye mchezo huo.

3 COMMENTS:

  1. Mwandishi picha uliyotumia tukueleweje? Je ni mashabiki wa yanga peke yao ndio walioingia uwanjani siku hiyo na hivyo kuchangia hizo pesa?

    ReplyDelete
  2. Hahaha kazi ipo kweli kk mpaka ukaelimika itakuchua miaka mingi

    ReplyDelete
  3. Hangover ya 4G. Msamehe ndio kwanza anazinduka.Kwani blogu hii hujaizoea?At least sasa habari za March 8 zimezikwa rasmi na Morrison wao.Shukrani kwa wachezaji wa Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic