July 15, 2020


MUDHATHIR Yahaya, kiungo wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.

Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila itamenyana na Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba.

Mchezo wake uliopita Katwila alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mble ya Mbao FC huku Azam FC ikitoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mwadui FC.

Mudhathir  amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja leo.

Mchezo wao uliopita wa mzunguko wa kwanza walipokutana walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa.

Timu hizi mbili zimekutana jumla mara 21 uwanjani ambapo Azam FC imeshinda mechi 10 huku Mtibwa Sugar ikishinda mechi 3.

Kwa upande wa sare zimepatikana jumla ya sare nane huku jumla ya mabao 44 yakipatikana ndani ya uwanja ambapo Azam FC imefunga jumla ya mabao 29 na Mtibwa Sugar wakifunga jumla ya mabao 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic