July 7, 2020


KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi bila ya kuwa na mkataba, hivyo kauli ya Bernard Morrison kuwa alicheza mechi mbili bila mkataba ni uongo.

Kamati ya katiba, sheria na hadhi ya wachezaji ya  TFF imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi kuu bila ya kuwa na mkataba.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Elius Mwanjala, ametoa kauli hiyo akitolea ufafanuzi alichokisema mchezaji Bernard Morrison kuwa aliitumikia Yanga katika michezo miwili bila ya kuwa na mkataba.

Mwanjala amesema kauli ya Bernard Morrison ni ya uongo kwa kuwa utaratibu wa wachezaji wote kucheza Ligi Kuu unafahamika, ni lazima awe na mkataba ili kupata usajili na uhalali wa kucheza ligi kuu.

Kuhusu  masuala ya mkataba wa Morrison, Mwanjala amesema wanasubiri kupokea baadhi ya nyaraka kutoka Yanga ili kufahamu uhalali wa mkataba wa miaka miwili ambao mchezaji anakana kuwa hajausaini.

Hata hivyo kamati hiyo imekiri kuipokea mikataba ya miezi sita na miaka miwili ya mchezaji huyo lakini wanasubiri kikao cha mwisho kuzipitia nyaraka zitakazowasilishwa na Yanga.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema wanaendelea kushughulikia malalamiko ya Yanga ambao waliyafikisha  katika kamati yao juu ya moja ya klabu nchini kutumika kumrubuni mchezaji wao Bernard Morrison kiasi cha kuukana mkataba wao.

Vilevile kamati imesema itatoa hukumu ya pamoja dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ambaye amelalamikiwa kuleta taharuki ndani ya Wekundu wa Msimbazi kwa kutangaza katika vyombo vya habari kuwa wamekamilisha mazungumzo na kiungo wao Clautius Chama, kinyume na utaratibu.

8 COMMENTS:

  1. Tangu awali nilijua TFF watamkana Morisson maana wakikubali kibao kitawageukia. Lakini kama morisson anaongopa basi aadhibiwe kwa kutaka kusababisha taharuki kwenye mwenendo wa ligi.
    Lakini pia nashangaa kuunganisha suala morrison kudaiwa kurubuniwa kuliunganisha na suala la Mwakalebela, huku ji kutaka kutanua magoli ili baadae wayamalize kwa kubalance mambo. Janja ya nyani kwisha jua.

    ReplyDelete
  2. Tff lazima wajitoe lawama kwani itabidi timu zidai pointi zao

    ReplyDelete
  3. Kama TFF hawajaweza kusema kama morisson ana mkataba na yanga wa miaka miwili, suala la kurubuniwa linatoka wapi. Yuko huru huyo kwa mujubu wa sheria za FIFA, labda watuambie wamejihakikishia kuwa alisaini mkataba wa miaka 2

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma vizuri pale. Ni kwamba wamekiri kuipokea mikataba yote miwili ya miezi sita na miaka miwili.

      Delete
  4. Ikiwa ni kweli Simba ilimrubuni Morrison, basi wakushtakiwa si Simba Bali ni mchezaji mwenyewe ambae Bila shaka ndie aliewambia Simba kuwa hakusaini mkataba mwengine na Yanga na ndipo dili lilipoanza, nasema tena ikiwa ni kweli Simba waliufanya maongezi nae

    ReplyDelete
  5. Eti wanasubir nyaraka zingne kutoka yanga ili watoe maamuz,inaonyesha waz tu kua huyo mchezaj Hana mkataba wa miaka 2

    ReplyDelete
  6. Nyaraka zipi tena wakati mikataba yote miwili wameshapokea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic