July 7, 2020


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kupoteza kwa kufungwa mbele ya Mbeya City ni makosa ya wachezaji wake ndani ya uwanja.

Jana, Julai 6, Coastal Union ilikubali kichapo cha mabao 3-1 na kuacha pointi tatu zikienda na maji.

Mgunda amesema kuwa imekuwa ni mwendelezo wa makosa ya wachezaji wake kushindwa kutimiza kile anachowaambia jambo ambalo analibeba yeye kwa kuwa ndiye mwalimu.

"Makosa ni yaleyale ambayo wachezaji wanayarudia hivyo sina uwezo wa kufanya tukiwa kwenye mchezo zaidi ya kuangalia namna gani tunaweza kuweka usawa.

"Bado simuoni mtu wa kumlaumu kwa matokeo ambayo tunayapata lakini lazima tuyafanyie kazi ili kuwa na mwendelezo mzuri," amesema Mgunda.

Coastal Union ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 33.

Kabla ya kucheza na Mbeya City ilitoka kupoteza mechi mbili kanda ya ziwa ambapo ilifungwa mbele ya Mbao FC na Alliance FC kote ilinyooshwa bao mojamoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic