July 14, 2020


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa suala la Bernard Morrison kiungo mshambuliaji kucheza chini ya kiwango na kuondoka baada ya dakika 64 alizotumia uwanjani linalihusu benchi la ufundi kwani wao ndio wanatambua ufiti wa kila mchezaji. 

Morrison mwenye mabao matano alitumia dakika 64 Julai 12 Uwanja wa Taifa wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 Kwenye mchezo wa hatua  ya nusu fainali dhidi ya Simba. 

Nafasi ya Morrison ilichukuliwa na mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana ambaya aliingia kumalizia dakika 26.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kuwa Morrison alisamehewa na mashabiki baada ya kufunga mbele ya Kagera Sugar ila kwa kushindwa kuonyesha kiwango bora kiliwakasilisha mashabiki.

"Suala la Morrison kushindwa kucheza kwa ubora hilo lipo ndani ya benchi la ufundi ambalo linatambua ni namna gani mchezaji alishindwa kuonyesha kiwango.

"Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar alifunga bao pekee la ushindi na mashabiki walifurahi na walimsamehe ila kwa kuwa ameshindwa kuonyesha kiwango kikubwa basi anazomewa,tutalifanyia kazi," amesema. 

Morrison baada ya kutolewa aliongoza safari mpaka nje ya uwanja ambapo alichukua bodaboda na kuelekea kusikojulikana.

10 COMMENTS:

  1. Nilichogundua hapa ni kuwa Morrison ni zaidi ya Yanga yaani ni mkubwa kuliko Yanga na wana muogopa sana...Kama GSM yuko nyuma ya hali ndio maana anapata kiburi cha kuwachezea viongozi wa Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kikwetu neno Mbilu linamaanisha 'MKUNDU"

      Delete
  2. Waseme tu hawanaa pesa za kuvunja mkataba wake

    ReplyDelete
  3. Muandishi kakosea. Morrison hakusamehewa lakini alizomewa

    ReplyDelete
  4. Mimi naona ajabu kwakuwa mpaka leo hii bado hawajaihusisha Simba kuboronga kwa wachezaji wao, hasa Morrisson

    ReplyDelete
  5. Simba haijawahi kuwa na uhusiano na sinema ya Morrison na Yanga. GSM ndio wenye filamu yao, walianza na kumwonesha kwenye media kuwa wameshamalizana naye kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili. Morrison alipokanusha hilo baadaye, wakabaki kusema mchezaji hajitambui. Alipogoma kwenda Shinyanga kocha mkuu alisema wameshamalizana. Alipoachwa kwenda Musoma walikuja kumbembeleza akaenda kucheza na Kagera. Mchelea mwana kulia...........

    ReplyDelete
  6. Morison ni zaidi ya yanga wanamuona mungu mtu kisa aliwafunga simba hako kagoli kamoja malipo yao wamekula 4G kama wamesimama

    ReplyDelete
  7. Wanamuogopa hadi Morrison kujuwa kuwa anaogopwa. Wao mboga wao wa kumuonea ni Molinga. Mara husifiwa, Mara kummaliza a nae aondoke, Mara huzomewa na huku yeye ndie bingwa wa kucheka na nyavu na haya ndio yanayowaumiza Gongonje. Hawakijuwi nini wakitakacho

    ReplyDelete
  8. Huyu mchezaji kwa ujumla hapa tz hatufai sio yanga tuu. Waachane nae. Wajiulize walimpataje na alitokaje South Africa? Arudi akacheze kwao Ghana nje ya hapo hawezi ana vinasaba vya kitapeli, ujivuni, dharau na kiburi

    ReplyDelete
  9. Wasijidanganye huyo Hana ubavu wa kutakiwa na Simba a hivo vituko angelivifanya Simba basi angelitimuliwa siku hiyohiyo hata ingelikua adaiwa milioni mia nne na tunaona Simba ya sasa hapana mmoja anaesumbuwa. Amani na raha imepamba kila pembe. Ati wanamtaka Chama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic