July 14, 2020

KIKOSI cha Azam FC kilicho chini ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania jana, Julai 14 kimewasili Morogoro ambapo kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Julai 15, Uwanja wa Gairo, mkoani Morogoro  mji kasoro bahari.

Azam FC itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC. 

Bao hilo la ushindi lilifungwa na mzawa, Andrew Simchimba Uwanja wa Azam Complex liliwafanya Azam FC kusepa na pointi tatu mazima.

Inakutana na Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila ambaye ametoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Mbao FC,  Uwanja wa Kirumba.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 38 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi zake 65 zote zimecheza mechi 34.

Katwila amesema kuwa ni mchezo muhimu kwake kushinda huku Cioaba akisema kuwa anahitaji pointi tatu pia.

1 COMMENTS:

  1. Azam Kazeni buti muchukue nafasi yapili na sisi tupo nyuma yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic