BAADA ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amefunguka kwa sasa kitu pekee kilichopo mbele ni kupeleka presha kwa wapinzani wao Azam FC katika kumaliza nafasi ya pili.
Mbelgiji huyo amesema kwa sasa hakuna chochote kilichopo mbele yao zaidi ya kupambana kuhakikisha wanamaliza kwenye nafasi hiyo ya pili baada ya malengo yao kushindwa kufikiwa.
Eymael jana alikiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Singinda United uliochezwa Uwanja wa Taifa na kuishusha Azam nafasi ya pili.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Arstica Cioaba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar.
"Kwa sasa hakuna cha kupoteza ni lazima tupambane kuipa presha Azam FC ambayo tunapambania wote nafasi ya pili na inawezekana kufanya hivyo.
'Bado ushindani ni mkubwa nasi pia tunapambana kufikia malengo yetu hivyo lazima tuwape presha wapinzani wetu ili kuona tunamaliza ligi tukiwa nafasi ya pili," amesema.
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65 zote zimecheza mechi 35.
0 COMMENTS:
Post a Comment