July 16, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa unashangazwa na taarifa ambazo huwa zinaeleza kuwa timu hiyo huwa inamwaga dawa kwenye mechi zake pamoja na kudaiwa kupulizia dawa kwenye AC jambo ambalo halina ukweli kwani wana kikosi kipana.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amekuwa akishangazwa na taarifa kuhusu AC pamoja na dawa kitu ambacho huwa hawafanyi.

"Unajua ukitoka nje utaskia sijui AC mara madawa yanawekwa duh mpaka anajiuliza hivi hawa watu wanajua upana wa kikosi cha Simba? Kuna watu wanajua kuuchezea mpira ila wanaishia benchi na sio ndani ya uwanja.

"Yupo Sharaf Shiboub yule jamaa kwa udambwiudambwi tu tuache uongo hafai anajua mpaka anapitiliza lakini ndani ya Simba anasugua benchi unadhani akienda Yanga ama Azam FC anaweza kusugua benchi?

"Hakuna kitu kinachoitwa dawa ndani ya Simba bali timu imara ndio maana tumetwaa ubingwa tukiwa na mechi mkononi sisi ni mabingwa na tunacheza kibingwa," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Enter your comment...dooooh ko ndo ufafanuzi huo tumieni tu madawa hii nchi yenu,ila mmefurahi saaana Mheshimiwa raisi kwa kumtangaza mkuu mpya wa mkoa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic